Kuna kitu nimekuwa nikiona lately. Watu wanakuja na "genius idea" halafu miezi sita baadae biashara imekufa kimya kimya, inakufa tu na mtu ana-move on.
I had this observation about this calorie tracking startup app by Zach Yadegari called cal ai https://calai.app, which he later sold kwa about over 100M$ after like less than 2yrs on market, kwamba Silicon Valley solves Silicon Valley problems, na ukijaribu let's say ku copy paste / likelihood hapa haifanyi kazi. You cannot tell a tanzanian kuna hii hapa App ya kutrack calories za chakula unachotaka kula kwa kupiga picha halafu the AI "describes your meal and get instant calorie and nutrient info." Then subscribe uanze kulipia solution. They don't need that, that's not considered a problem on this land. There is no ecosystem that supports that kind of innovation, Hiyo imenifanya nifikirie zaidi. Sio tu apps za teknolojia, hata biashara za mtaani, za kawaida kabisa, zina mfano huu huu wa kufa kimya.
Kwa hiyo nataka kujua kutoka kwa watu wenye uzoefu wa kweli (real experience):
Je, kuna wazo la biashara ambalo umeliona likijaribiwa na watu wengi (say 5+ tofauti tofauti) kila mmoja akiamini yeye ndiye atafanikiwa tofauti na wale wengine, halafu wote wanashindwa kwa sababu ile ile moja?
Sio ile ya "hakuna soko" tu, nataka ile specific killer, kitu ambacho hakiko kwenye business plan yoyote lakini ndicho hasa kilichoua biashara. Mfano inaweza kuwa suala la supply chain, cash flow, wateja kutokuwa tayari kulipa bei fulani, ushindani wa watu wasio rasmi, ama hata utamaduni wa jinsi watu wa hapa wana-consume kitu fulani.
Nauliza hii kwa sababu naona watu (mimi nikiwemo) tunapenda kuzungumzia mafanikio zaidi kuliko sababu za kushindwa. Lakini ukweli ni kwamba ukisikia mtu mmoja alishindwa, unaweza kudhani ni bahati mbaya yake tu. Ukisikia watu watano wameshindwa kwa sababu ile ile, hapo ndipo unagundua kuna kitu cha kimuundo, sio bahati mbaya.
Kama umeshawahi kujaribu mwenyewe, au umeona rafiki au ndugu akijaribu na kushindwa, naomba ukae chini uniambie ilikuaje kwa undani. Sitaki tu jina la biashara, nataka hicho kitu specific kilichoua, na kama unaweza, hicho kingekuwa tofauti gani kama mtu angekifanyia kazi mapema.